side ads

TATIZO NI DAWA AU KWAKUWA ZIMETOKA UCHINA?

Kuna baadhi ya nyakati ambapo mtu unaweza ukajikuta unacheka si
kwakuwa unafuraha, laa. Bali kwakuwa huna namna. Ndio, maumivu
yanapozidi sana, ukajikuta umeshalia sana na haijasaidia kitu, si bora
ujifariji mwenyewe kwa kujibaraguza kucheka walau kidogo?

Dawa za kuongeza au sijui kukuza na kunenepesha baadhi ya viungo vya
binadamu, ndio gumzo kuu kwa sasa. Kila kona ya Tanzania, habari ni
hiyo. Na kwakweli, kama ni umaarufu, basi dawa hizi hivi sasa ndio
zinaongoza.

Jambo moja tu ambalo limekuwa likiniumiza kichwa katika mjadala huu
ulioliteka taifa, ni swali la JE, TUNA SABABU ZA MSINGI ZA KULIFANYA
LIWE ISSUE KUBWA KIHIVYO? Na kama ipo hiyo sababu ni ipi?

Najiuliza hili kwakuwa, hapa nilipo mbele yangu niko na gazeti, ambalo
katika ukurasa wake wa matangazo madogo madogo, umejaa kwa kiwango cha
asilimia 70, matangazo ya madaktari pori na mitishamba yenye kutibu
UKIMWI, kuongeza ukubwa wa hips, maumbile ya mwanaume, kumrejeshea
mwanamke ubikra nk.

Kuna tofauti moja tu ninayoiona kati ya dawa hizi na zile ambazo hivi
sasa zimekuwa gumzo la nchi. Na tofauti hii ni ile ya maeneo
zinakotokea dawa hizi. Ni kuwa aina ya kwanza imetoka nje ya nchi,
imepanda au kupandishwa kwenye ndege toka China hadi Tanzania, ilhali
ya pili imetokea hapo jirani tu kwenye kilima tunakokata kuni.

Hapa ndipo nashikwa na kizunguzungu kwakweli. Maana siioni mantiki ya
serikali yetu kupitia mamlaka zake mbalimbali hivi sasa kuanza kutumia
muda wao mwingi kupiga marufuku dawa hizi, wakivamia maduka ya watu
ili kuzisaka wazichome moto sijui, ilhali ikiwaacha wale waliochafua
miji kwa vitamba vyenye kutangaza dawa hizo hizo wakipeta tu.

Na hapa ndio ninapojiuliza kuwa homa hii iliyotukumba ni kwa minajili
ya kuwakinga watu wetu kweli au ni kwakuwa tu dawa hizi zinatoka
China? Au wakubwa wamegundua ni biashara inayolipa sana kwahiyo
wanaitengenezea mazingira ya wao tu ndio wawe wanaifanya tena kwa
maslahi makubwa zaidi?

Anyway, mie simo. Najiuliza tu

--
Sent from my mobile device

Msangi, R.S

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Anonymous said...

Watu wajifunze kuuliza faida na hasara zake kabla ya kutumia, ila kwa jamii ya watu wetu ambao elimu bado haijamwezesha kudadisi, kuchambua na kupambanisha ukweli wa mambo, wengi watalizwa. Wasomi, hii ni nafasi ya kurudisha faida ya usomi kwa kupambanua mambo kinagaubaga.

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! Mbona maswali yanazidi kuwa mengi kuliko uwezekano wa majibu?
Lakini swali hapa ni kuwa inakuwaje sasa hivi hizi dawa zinapata umaarufu kiasi hiki ilhali kulikuwa na nyingine nyingi za namna hii?
Ni kweli kuwa dawa hizi zina matatizo? Na kama ni kweli, basi tatizo ni aina ya dawa ama aina ya matibabu yanayotibiwa? Na kama ni aina ya matibabu, ni kwanini hawakukataza tangu awali? Na kama ni dawa, inakuwaje wanasubiri mpaka ziwe maarufu ndio wazikataze?
Hapa wala si kumjali "mlaji" bali ni kujisafishia njia ya mwakani. Ni kama alivyosema Kaka Kamala (http://kamalaluta.blogspot.com/2009/08/maisha-bora-yashafika-hamyaoni.html) kuwa MAISHA BORA NDIO YANAANZA KUONEKANA NA NI WAKATI WA KU-TAKE ADVANTAGE.
Nami naacha