side ads

NANI MWINGINE WA KULIANDIKIA TAIFA HILI HISTORIA?

Baada ya hayati Mwl. Nyerere, aliyeuhangaikia uhuru wa nchi yetu (japo ni wa bendera) na hatimae mzee Mwinyi, aliye-reintroduce mfumo wa vyama vingi japo ni chini ya robo ya Watanzania tuliokuwa tumeukubali, ni kama nchi hivi sasa imekosa watu wa kuiandikia historia upya.

Matarajio makubwa ya Watanzania yalikuwa kwa rais wa sasa, Jakaya Kikwete. Lakini wakati miaka yake mitano, ikielekea magharibi hivi sasa, hakuna hata dalili ya yeye japo kuongeza tu kurasa mpya, achilia mbali kuiandika upya.

Huyu alikuwa mtu aliyebeba imani kubwa sana ya Watanzania ambao tulitaraji kwanza kabisa angehakikisha mchakato wa kubadili/kuboresha katiba unaenda kasi ili waliotutafuna katika awamu za nyuma wanawajibishwa (maana hawawezi kujiwajibisha).

Huyu alikuwa mtu ambaye Watanzania wengi walitaraji atende katika matamshi yake, na si kutenda kinyume na kauli zake.

Huyu alikuwa mtu ambaye tulitarajia hivi sasa awe amenuniana na wanyonyaji wanaojiita wawekezaji, awe amewatimua kama si kuwawajibisha kwa kuwaibia Watanzania.

Tulitarajia kuwa awe ametekeleza ahadi yake ya kuhakikisha waisilamu hawageuki kuwa mjadala wa Bungeni hivi sasa.

Tulimtaraji awe mfano wa watakaomfuata katika kuitekeleza sheria kwa kuwawajibisha watendaji ambao wamewahujumu Watanzania kwa kutumia fedha zao kupata elimu ambayo wameiweka mifukoni mwao na kujaza tamaa vichwani mwao.

Tulimtarajia kwa mengi kwakweli, lakini inavyoonekana ni kuwa ameukosa ujasiri huo. Amekosa muda wa kupambanua tofauti baina ya Watanzania wenzake wanaomuamini dhidi ya ile ya marafiki.

Matokeo yake, hali ndio kama ilivyo. Maisha bora kwa kila Mtanzania, umekuwa wimbo ambao hauchezeki hivi sasa.

Hapa ndipo wasiwasi mkuu unapokuja na tukaanza kujiuliza. Je, hofu hii aliyonayo JK, inatokana na nini hasa? Kipi kinamshinda au wapi anakwama katika kutengua maamuzi ambayo yalifanywa awali lakini anajua wazi yanawagharimu Watanzania?

Ni kwakuwa alikuwa sehemu ya maamuzi hayo au? Na hata kama ni hivyo, je, suluhisho ni kusahihisha makosa kwa kutenda makosa zaidi?

Kama JK, anashindwa, na ndio dalili zilizopo, nani wa kuandika upya historia ya ukombozi wa Mtanzania?
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

James wa Matukio said...

kiiukweli ni kwamba hakuna

serikali hii sanasana inaweza kujiandikia historia ya kuwa serikali pekee ambayo iliingia madarakani kwa mbwembwe nyingi sana huku ikiwa imebeba kila tumaini la Watanzania, lakini ikawaangusha....hapana, ikawachinjia baharini kama si kwenye mto wenye maji yaendayo kasi sana