side ads

NINI KILIIKUMBA Air France Flight 447, USAFIRI WA ANGA UNGALI SALAMA?


JE, usafiri wa anga ndio njia salama zaidi ya kiusafiri kuliko nchi kavu na majini? Hili ndio swali ambalo limeiteka dunia hivi sasa, ikiwa ni takriban siku mbili na ushee sasa toka ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, iliyokuwa na abiria na wafanyakazi wapatao 228 ndani yake, ipotelee katika anga la bahari ya Atlantiki, ikiwa katika safari ya kutoka Rio de Janeiro kuelekea Paris.

Makundi ya wataalamu sehemu mbalimbali duniani wamegawanyika katika makundi madogo madogo yenye kutofautiana kimtizamo kuhusu nini hasa kilichoikumba dege hiyo, hadi kupoteza mawasiliano na waongoza ndege toka viwanja mbalimbali. Wapo ambao wangali wakijiuliza NINI HASA KILIIKUMBA NDEGE HIYO?

Wakati mtandao wa LIVE SCIENCE, ukichapisha habari ndefu kuelezea kuwa licha ya kilichotokea kwa ndege hiyo, USAFIRI WA ANGA BADO NDIO SALAMA ZAIDI, kundi jingine la wataalamu limekuwa likijadili zaidi kuhusiana na dhana hiyo ya usalama wa usafiri wa anga, ambapo wanajiuliza JE, BADO USAFIRI WA ANGA NI SALAMA ZAIDI YA NCHI KAVU? Aidha, kufuatia tukio hilo, wataalamu pia wamekaa chini na kuchanganua UWEZEKANO WA KUPOTEZA MAISHA, kwa wasafiri wa njia ya anga.


Je, ni yupi aliye sahihi zaidi ya mwenzie? Bila shaka huu ni mjadala mzuri sana wa kufuatilia kwa kina. Na wakati tukiendelea kufuatilia mjadala huu, pengine ni vyema tukajipatia ufahamu wa namna makundi ya ndege (wanyama), yanavyoweza kuangusha ndege (chombo cha usafiri ). Bongeza HAPA, kusoma taarifa hiyo. Na wakati huo huo bonyeza HAPA, kujua namna ambavyo radi, ngurumo na hali nyingine mbaya za hewa zinavyoweza kusababisha hatari kwa usafiri wa angani.

Na kwa kadiri masaa yanavyozidi kusonga mbele, tayari wataalamu wameshaanza kuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kuokolewa kwa mtu yeyote akiwa hai kutoka katika ndege hiyo. Na ikiwa hakuna atakayeweza kuokolewa akiwa hai kama wasiwasi unavyozidi kutanda, basi tukio hili litakuwa ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba tasnia ya usafiri wa anga tangu mwaka 2001. Soma habari kuu kuhusu kupotea kwa ndege hiyo, kupitia HAPA na habari ya kwanza kutoka jukwaani kuhusu tukio hilo, kwa kubonyeza HAPA. Kujua aina, mashirika na safari za ndege zilizo salama zaidi bonyeza HAPA.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli kusafiri yataka moyo. usafiripo usiwaza nitakufa we safiri tu. Nawapa pole wafiwa wote ni jambo la kusikitisha pia la ajabu.

Anonymous said...

I have removed this phrase