side ads

228 WAHOFIWA KUFA BAADA YA NDEGE KUPOTEA


Kuna wakati hapa kati kati, usafiri wa anga, ulikuwa ukichukuliwa kama ndio usafiri ambao usalama wake ni wa uhakika zaidi kulinganisha na usafiri wa nchi kavu au ule wa majini. Hii ilitokana na ukweli kuzidi iri wan chi kavu huku pia dunia ikiwa iko katika zama mpya na za aina yake za uharamia katika vyombo vya usafiri vya majini.

Lakini, tayari wadau na wadadisi wa masuala ya usafiri wameshaanza kuanza kukokotoa usalama uliokuwa ukisemekana kuwepo katika vyombo vya usafiri vya angani, kufuatia ajali za ndege nazo kuzidi kushika kasi ya ajabu. Na miongoni mwa matukio ambayo yamesukuma mchakato wa wadau na wadadisi hao, ni ajali iliyotokea leo iliyohusisha ndege aina ya Air Bus A330, mali ya shirika la ndege la Ufaransa.

Ndege hiyo inayotajwa kuwa ilikuwa na umri wa miaka mine tu, ilikuwa na abiria 216 na wafanyakazi 12, ilikuwa ikitokea Reo de Janeiro, kuelekea Paris, ambapo inasemekana kuwa ilipata matatizo wakati ilipokuwa ikikatiza katika ukanda uliokuwa na radi na ngurumo kali katika bahari ya Atlantiki. Soma habari hii kwa kina kwa kubonyeza hapa. Tizama picha ya video kwa kubonyeza hapa
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

4 maoni:

James said...

ajali...ajali....ajali. Ni kama dunia haina kitu kilicho salama kwa sasa. nilikuwa nafikiria eee... labda turudi zama zile za kale, lakini mh!! nazo wazee wetu si walikuwa wanaliwa sana na wanyama wakali wakati wakisafiri masafa marefu. Hivi tufanye nini sasa?

haruna said...

Msangi, mbona hiyo video yako haichezi?

Anonymous said...

this is the breaking nyuuuuuuuuuuuuuuuz

Ramadhani Msangi said...

Mh!! giyo video kutocheza ndugu yangu, inawezekana kabisa ikawa ni tatizo la kompyuta unayoitumia. Maana nimeichukulia katika mtandao wa yahoo. Nasikitika kwakweli kuwa siwezi eleza hilo kiutaalamu zaidi