side ads

Wenye makampuni ya simu za viganjani, acheni tabia hii.

Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa hivi sasa, kwa watumiaji wa
mitandao mbalimbali ya hizi simu za viganjani, kupokea taarifa za kila
aina kulingana na wanavyohitaji na hata zingine wasizohitaji.

Kuanzia utabiri wa nyota mpaka hali ya hewa. Ratiba za safari,
vichekesho, promosheni mbalimbali nk. Ilimuradi kila kampuni
inajitahidi kujipambanua toka kwa mshindani wake. Na cha kufurahisha
zaidi ni vile taarifa hizo zinavyopatikana kwa wepesi wa hali ya juu.

Unaweza kukuta mmekaa mahali mkiwa kikundi cha watu na katika wakati
fulani ndani ya dakika chache sana, wote mkawa mmepokea ujumbe kuhusu
promosheni fulani. Kwakweli inapendeza kuona watoa huduma hawa
wanavyokuwa wabunifu wa huduma za ziada/nyongeza na kuwaarifu wateja
haraka sana.

Hata hivyo kumekuwa na tabia ya watu hao hao ya kuwa wazito katika
kutoa taarifa kuhusiana na tatizo lingine lolote. Ni kwanini? Mtu
nakatwa hela ili niweze kupata huduma fulani, lakini unakuta naambulia
patupu siku nzima. Si dharau hizi ni nini jamani? Kwanini kasi ya
kututambulisha promosheni, isitumike katika kutupatia wateja taarifa
za tatizo hadi tena mtu kulazimika kuwapigieni simu huduma kwa wateja,
ambazo nazo zinakatwa hela?

Tabia hiyo jamani haifai. Inakera, inatukwaza wateja wenu.

--
Sent from my mobile device

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: