side ads

INGEKUWA VIPI KAMA........................

Hivi, ingekuwa vipi kama leo nisingetembelea maskani ya zamani ya Ndesanjo Macha na kukuta ile kauli mbiu aliyoinukuu toka kwa Indya Nkya? Eti jamaa anatamani kipindupindu kingie Ikulu!, waswahili tuna mambo jamani, mh!! Anyway, lakini unadhani ingekuwa vipi kama kipindupindu kingeingia pale maskani ya JK?

Kisha nikakumbana na taarifa ya wanafunzi wa chuo cha Mkwawa, kuwa wanashindia mapera kwa ulanzi. Jamani!! Hivi ingekuwa vipi kama taarifa hizo zingekuwa za kweli, halafu mapera yenyewe yawe magumu magumu hivi kasha ndio washushie na ka-ulansi kwa mbaaaali. Unadhani ingekuwa vipi mtu wangu?

Tuyaache hayo bwana, maana waswahili hatuishiwi vijambo. Tuzame kwenye somo letu la msingi la leo. Hivi unadhani ingekuwa vipi kama waswahili tungeacha utamaduni wa kujibu maswali kwa staili ya kuuliza swali jingine?

Ingekuwa vipi kama leo hii Lowasa, angelikuwa bado ndani ya system? Je, zile mvua za kutoka ughaibuni zingekuwa zishawasili na kuanza kumwaga neema ndani ya Bongo au? Na wale wataalamu wa kulima uyoga nao, wangekuwa washatutembelea au?

Ingekuwa vipi kama Dk. Slaa, angekuwa ndio yuko pale magogoni instead of JK, na kisha Freeman Mbowe, akawa ndio yuko katika position ya mheshimiwa Pinda? Unadhani leo hii kesi za EPA na BOT, zingekuwa bado zinaendelea kusua sua kwa mashahidi kufa na mahakimu kuumwa ghafla?

Ingekuwa vipi jamani, ikiwa leo hii, Mrisho Mpoto angelikuwa ndio waziri wa utamaduni, burudani na michezo, huku malkia Sophia Kessy, akiwa ndio naibu wake? Na ingekuwa vipi kama Fetty, angekuwa ndio spika wa Bunge halafu wakati mimi ndio katibu wa pale mjengoni? Ingekuwa poa sio?

Ingekuwa vipi kama U-Mungu, ungekuwa ni cheo cha kugombewa kama ubunge, udiwani au ujumbe wa nyumba kumi na kasha nanihii…(huyo huyo jirani yako hapo), ndio akagombea na kushinda kasha akatawazwa kuwa Mungu mpya?

Ingekuwa vipi kama asingetokea mtu aliyebuni, kutengeneza na kasha kuziachia wazi blogi kwa ajili ya kila anayehitaji? Ingekuwa vipi kama leo hii tusingekuwa na simu za mkononi? Unadhani maisha yangekuwa mazuri sana au mabaya zaidi ya yalivyo sasa?

Ingekuwa vipi kama nawe ungejiuliza maswali kadhaa juu ya ingekuwa vipi, na kisha Watanzania nao wakakujibu kwa staili ile ile ya kuuliza maswali zaidi?
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

4 maoni:

Koero Mkundi said...

NAMI BADO NAJIULIZA INGEKUWA VIPI?
HAYA MASWALI YANAHITAJI TAFAKURI. ILA SIASA KAKA MSANGI HAZITABIRIKI, UNAWAKUMBUKA KINA MULUZI, CHILUBA, KIBAKI.
NADHANI SIHITAJI KUKUELEZA LOLOTE KUWAHUSU, JUST FILL THE BLANK SPACE....

Yasinta Ngonyani said...

Nanukuu "Ingekuwa vipi kama asingetokea mtu aliyebuni, kutengeneza na kasha kuziachia wazi blogi kwa ajili ya kila anayehitaji? Ingekuwa vipi kama leo hii tusingekuwa na simu za mkononi? Unadhani maisha yangekuwa mazuri sana au mabaya zaidi ya yalivyo sasa?" Nadhani maisha yangekuwa mazuri zaidi, watu wangekuwa wanatembeleana zaidi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Sasa hivi wengi muda wao mwingi wana kaaa kwenye kompyuta. Ila kitu komoja ambacho ni kizuri ni kwamba kublogi kumeltufanya wengi tupate marafiki ambao tunao leo kwa hiyo kwa namna nyingine ni vizuri. nimejibu hilo tu kwani kulikuwa na nyingi INGEKUWA VIPI?

Anonymous said...

Twende mbali zaidi,tujiulize hivi ingekuwa vipi kama Dar es Salaam ingekuwa kama New York (bila vumbi) hii michongo yakutokea ya ndugu zangu Wachaga kuanza kwa ushoe shiner kisha kaduka kadogo na baadae Duka kubwa na kumwajiri ndugu naye akafungua lake zingekuwepo?
by Anold kayanda

Anonymous said...

mi naona kama ingekuwa bado maswali mengi tu ambayo tunajiuliza kila wakati ukizingatia njaa ndio zimezidi ingekuwa

kaka pole kwa kuwaza
sophie malkia