side ads

HAPPY BIRTHDAY SOPHIA KESSY


Ni kweli kabisa kuwa wapo wengi ambao ulizaliwa nao, lakini leo hii hatunao katika ulimwengu huu wa manani. Ni wazi kabisa kuwa wapo wengi walizaliwa baada yako, lakini hawakuweza kufikia siku ya leo kwa utashi wa aliyetuumba. Hivyo basi ni faraja kubwa sana kwako wewe kufika siku hii na katika mwaka huu.

Si kwamba umependelewa sana...laa. Isipokuwa Mungu amekuweka hai hadi leo hii kwa makusudi kabisa. Tumia muda wako mwingi kumkumbuka Muumba wako, Sali sana kabla hajaamua kuchukua pumzi alizokuruzuku. Fanya kazi kwa bidii, endelea kumheshimu kila aliye mbele yako, maana Mungu hakutuumba sisi wanadamu kwa usawa, bali kwa uadilifu mkubwa sana.

Kwa niaba ya wadau wa Jukwaa la Uchambuzi, na kwa niaba yangu binafsi, tunapenda kukutakia maadhimisho mema ya siku yako ya kuzaliwa. Mungu akujaalie uhai mrefu zaidi na zaidi.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: