side ads

Special Arshavin on a Special Night at a very Special place


Hallow and welcome to Anfield, a very special place on a very special night – Mtangazaji wa luninga aliyetangaza pambano baina ya Liverpool na Arsenal, Jumanne ya April 21, 2009.

Wakiwa wanakosekana Manuel Almunia, Gael Clichy, William Gallas, Robin Van Persie na Emanuel Adebayo na baada ya kusoma orodha ya wachezaji 11 waliokuwa wakianza pambano hilo, huku Edwardo Silva na Theo Walcott, wakionekana kuanzia benchi, ni mashabiki wachache sana wa Arsenal, ambao wangeweza kusadiki maneno hayo hapo juu ya mtangazaji.

Special night kwa Arsenal iliyoonekana dhaifu kiasi kile dhidi ya Liverpool, ambayo kimsingi mchezaji wa muhimu pekee aliyekuwa akikosekana alikuwa ni nahodha wao Stephen Gerrard! Hapana, ilihitaji uwe na moyo wa ziada kusadiki maneno hayo kwakweli. Ilihitaji mtu mwenye imani ya kweli ya kisoka ili kuweza kuyasadiki.

Lakini wafuasi wa kweli wa soka hupenda kusema kuwa, kuna vitu fulani fulani adimu sana ambavyo ndivyo vyenye kuufanya mchezo wa soka uwe wa aina yake na wenye kuvutia kwa namna ya kipekee, humu duniani (maana sijui kama ahera nako upo au laa). Na bilashaka, matokeo ya pambano lile, yalikuwa miongoni mwa vitu hivyo vichache vyenye kuipa soka upekee wa aina yake.

Na bilashaka, baada ya dakika zile 96, za pambano lile lililoishia kwa matokeo ya bao 4-4, na ambalo lilikuwa na lingali linachukuliwa kuwa lilikuwa muhimu katika kuamua hatma ya wenyeji Liverpool, kunyakua ubingwa katika msimu huu, ikiwa ni miaka 19 toka wautwae mara ya mwisho, kila mtu anaweza kukubali kwa 100% au hata zaidi, kuwa mtangazaji yule, alimaanisha alichokuwa anakisema.

Kwa thamani ya vikosi vya wachezaji, kuna tofauti kubwa sana baina ya wale wa kikosi cha Arsenal, na wale wa timu za Manchester, Liverpool na Chelsea. Kikosi cha Arsene Wenger kina thamani ya karibu nusu ya vikosi vya kila timu hizo zingine. Lakini kwamba wameweza kuchukua pointi katika kila mechi waliyokutana na wapinzani wao hao, ni faraja kubwa sana kwa Arsenal.

Yes, Anfield on April 21st was a very special place on a very special night, hususan kwa kiungo mshambulizi wa kirusi, Andrei Arshavin. Najua mashabiki, wachezaji na hata mameneja wa timu za Manchester na Chelsea, hivi sasa wako matumbo joto. Poleni sana….huo ndio utamu wa soka, na mambo hayo ndio yanalifanya soka kuwa la kipekee kwa namna ya kipekee pia.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: