side ads

HERI YA PASAKA WANA JUKWAA WOTE


Leo ni siku ya Pasaka, siku ambayo wakristo kote duniani, wanaungana kukumbuka mateso aliyoyapata Yesu Kristo, pale aliposulubiwa msalabani na watu waliokuwa wakimpinga. Ni siku nzuri sana kwa ajili ya kutafakari kuwa sisi tunafanya nini kwa ajili ya kumrudia Mungu wetu? Tunafanya nini kuifanya dunia kuwa sehemu ambayo inastahili mwanadamu kuishi na kuyafurahia maisha? Je, tuna kina nani ambao leo hii wanafuata uelekeo wa Yesu, ambaye alikubali kufa kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu?

Wakati imeshakuwa jambo na utamaduni ambao umezoeleka duniani hivi sasa, kwa watu kutumia nyakati kama hizi kufanya mashindano ya kumkubali shetani, kwa kushiriki matukio mbalimbali ya kishetani, pengine ni vyema hivi sasa, tukabadilika na kutumia nyakati kama hizi kwa kutafakari ni wapi dunia ilitoka, wapi ilipo hivi sasa na tunaipeleka wapi?

Kwa niaba yangu mimi binafsi na wale wote wenye kunihusu, napenda kuwatakia wadau wote HERI YA PASAKA.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Yasinta Ngonyani said...

Nimechelewa kidogo, Lakini nasema tu Heri ya Pasaka nawe pia na familia yako. natumai umekuwa na muda mzuri.