side ads

maswali ya kizushi + politiki za wana-JUMUWATA

Mbona wakati unalo gari hawakukuuliza kuwa unalo, lakini unapotembea kwa miguu ndio wakuulize gari liko wapi? Haya ni miongoni mwa maswali yanayonishangaza kidogo. Hebu yacheki mengine kupitia hapa, kasha tusaidiane kujadili, nini chanzo
======================.

Kila ninapojaribu kufuatilia mjadala aliouanzisha Bwaya kuhusu JUMUWATA, nazidi kupata mambo mapya yenye kufurahisha na kusisimua sana. Na hapa ndipo ninapobaini kuwa kauli mbiu ya JUMUWATA, ya “majadiliano ndio njia bora ya kuelekea maendeleo endelevu”, ilitakiwa pia kuongezewa maneno haya “na kubaini uwezo wa watu kufukiri mambo”

Kila ninavyozidi kufuatilia mjadala ule pia ndivyo ninavyokumbuka kichekesho cha rafiki yangu mmoja alowahi kunitania akisema eti “Muisilamu akibatizwa na kuwa mkristo, hujitahidi kuwa mkatoliki zaidi kuliko hata Papa".

Ningeweza kusema kuwa nimeshangazwa na maoni ya mchangiaji mmoja aliyedai Mwenyekiti wa JUMUWATA, “alijificha” hadi ulipoibuliwa mjadala, huku mwingine akisema uongozi ung’oke usisubiri kupinduliwa sijui kuaibishwa vile?. Lakini nitasema sikushangazwa na michango hiyo kwa ujumla na nitasema kwanini.

Kwanza kabisa, miongoni mwa malengo ya Blogi kwa ujumla wake, ni pamoja na kutoa jukwaa huru kwa watu kutoa maoni yao (ubora wa mawazo au maoni, hutegemea kiwango cha busara cha mtu mwenyewe kufikiria) na vile vile, miongoni mwa malengo ya JUMUWATA, ni pamoja na kutoa fursa ya kila Bloga wa Kitanzania, kuwa na uwanja wa kushiriki majadiliano kwa kuamini kuwa majadiliano ndio njia muafaka ya kuendelea maendeleo endelevu.

Pili, sikushangazwa sana na maoni yale, kwasababu miongoni mwa magonjwa ambayo asilimia kubwa ya Watanzania tunaugua, ni ugonjwa wa uanasiasa. Ugonjwa ambao unamfanya kila anayeugua kudhania kuwa kila kitu kinaweza kwenda kwa kauli/tamko/utashi au maono yake, bila kuangalia changamoto kadhaa ambazo zinaweza kumkabili.

Simulizi liko kama ifuatavyo

Wakati watu kadhaa walipopata maono ya umuhimu wa kuwepo kwa Jumuiya, walichoamua kufanya kwa wakati huo kwa kuanzia ilikuwa ni pamoja na kushirikisha wadau zaidi ya asilimia 75 waliokuwa wakishiriki kublog kwa wakati huo. Kwa bahati mbaya sana, mwitikio wa walioshirikishwa kwa wakati huo ulikuwa zaidi ya kutokuridhisha. Lakini hilo halikuwakatisha tama waliokuwa wamibua wazo hilo.

Katika kipindi chote cha michakato kadhaa iliyofanywa na waliokuwa wakifikiria katika uelekeo huo, ushiriki wa watu ulikuwa ni duni zaidi ya maelezo pia, na ilipofikia mahali ambapo changamoto mbalimbali za kimaisha ziliongezeka kwa waliokuwa wakiendesha gurudumu hilo, ndio mambo yakawa mabaya zaidi maana hawakuwahi hata kujitokeza watu kutaka wabebeshwe wao makasia ili waendeleze safari ya jahazi hilo, ukiachilia mbali watu waliokuwa wakipiga blah blah mbalimbali kama baadhi wanavyofanya katika kuchangoa hoja ya Bwaya kule maskani kwake.

Kama wapo watu ambao walikuwa serious na wanachokiongea, waliowahi hata kuthubutu kutumia sehemu ya kile walicho nacho katika kuhangaikia hili, nitaomba wajitokeze hadharani tusutane. Na hapa namaanisha waliokuwa kweli serious, sio wale wa blah blah za hapa na pale.

Na sasa kaibuka mtu katoa hoja, basi ndio waliosilimu wanataka kuwa wakatoliki zaidi ya Papa. Inac hekesha kwakweli. Politiki kama kawaida. Hivi inapotokea mtu akaibua hoja ya kufufua kitu ambacho kilikuwa kinalegalega mahali, wenye nia ya kufufua wanaanzia wapi kama kwanza si kupata taarifa ya jambo hilo lilipoanzia hadi lilipokwamia au kufia?

Hivi inapotokea mtu kukurupuka na kudai waondoke viongozi wasisubiri kuaibishwa sijui kupinduliwa, mtu huyu ana uhakika kuwa anaiujua katiba ya JUMUWATA, kuwa inasemaje kuhusu uongozi na namna ya kuuondoa uongozi? Aliifuata na ikashindikana hadi kuanza kile ninachothubutu kukiita longolongo za kipolitiki?

Ni nani alitoa ombi au tamko kuwa uongozi uondoke maana umeshindwa akapingwa hadi ifikie hatua ya kudai wasisubiri kuaibishwa?

Tuache longolongo watu wangu. JUMUWATA ipo wazi kwa kila mtu kujiunga na kushiriki uongozi tena kwa uhuru mkubwa sana, maana hiki si chama cha kisiasa. Kuanza kukurupuka na kutoa matamko ya kisiasa, hakuwezi kutufikisha popote pale. Tutaishia kulumbana badala ya kujadiliana, na hatua hii sidhani kama itakuwa muafaka kwa JUMUWATA, au yeyote mwenye malengo kama ya liyokuwa yanakusudiwa na jumuiya hii.

Tunaweza kuwa tunaandika sana habari za siasa na wana siasa, lakini hilo halimaanishi kuwa tumekuwa wanasiasa. MJADALA UENDELEE
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Bwaya said...

Ndugu Mwenyekiti,

Awali ya yote hongera kwa kuweza kuchukuliana na tofauti ya mawazo, na kuweza kujibu baadhi ya hoja zilizojitokeza kwenye mjadala ule. Naamini unaendelea na hilo.

Niliona umuhimu wa kuwa na mjadala wa namna ile, kwa mapenzi niliyonayo kwa jumuiya. Nia hasa ilikuwa walau kuwaleta wadau wapya na wakongwe pamoja ili kwa pamoja, tuweze kuiimarisha upya jumuiya yetu.

Ndugu mwenyekiti,

Naamini kwamba unatamani pia kuona msisimko uliokuwepo enzi zile unarudi. Hamasa zile zinafufuka. Na umoja ule unarudi. Ndivyo ilivyo. Na ndio maana hukusika kuchangia maoni yako pale hata kama wapo wadau ambao walionyesha kuushambulia uongozi uliopo. Nikupongeza kwa hilo.

Tulipo, ndugu mwenyekiti, tunaweza kabisa kuurudisha tena msisimko ule. Tusahau yaliyopita. Tuanze upya.

Nimeziona jitihada za Katibu kuiamsha blogu ya jumuiya. Sijui alipofikia, lakini naona kuna umuhimu mkubwa sana wa blogu ile kuanza kupumua.

Hiyo itasaidia kutuunganisha na kutuwezesha kujadiliana pale.

Hiyo, bila shaka itakuwa hatua muhimu katika mchakato huu.

Nikushukuru tena ndugu mwenyekiti.