side ads

JUMUWATA: ilipotoka, ilipo na hatma yake

Hii ni sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala kadhaa ambazo nimeazimia kuziandaa, kwa lengo la kujadili mustakabali wa JUMUWATA. na ni vyema tu ieleweke kwa kila mdau hapa kuwa, nitakuwa nikifanya hivyo nikiwa nimevaa kofia ya Uenyekiti wa JUMUWATA, mbali ya kuwa mmoja kati ya wanachama waasisi wa Jumuiya hiyo.

Nianze kwa kumshukuru sana ndugu Bwaya, kwa kuanzisha mjadala huu katika maskani yake ambapo aliandika kwa ufupi sana lakini katika maneno ambayo yalivuta wachangiaji wengi kuhusu JUMUWATA, akisema:

Ningependa kumwomba mheshimiwa Katibu Mtendaji wa JUMUWATA ruhusa ya kuuliza swali hili. Tumefikia wapi na ile Jumuiya ya Wanablogu Tanzania? Mnaonaje
tukifanya mjadala wa wazi kuhusu 'ufufuaji' wa jumuiya yetu? Jamani yasijeyakawa
yale ya mwaka elfu tisa mia sabini na saba.

Kama ambavyo nimegusia hapo juu, maneno ya ndugu Bwaya, yalikuwa machache sana lakini ambayo yalivutia wachangiaji wengi sana, huku kila mchangiaji akitoa mtazamo wake kwa mujibu wa vile anavyoelewa au asivyoelewa kuhusu JUMUWATA. Na katika mfululizo wa makala zangu, nitajitahidi sana kujibu hoja mbalimbali ambazo zimetolewa na wadau waliochangia makala ya ndugu Bwaya.

Miongoni mwa changamoto ambazo nitapenda kuzigusia katika makala hizi, ni pamoja na hii ya KOERO MKUNDI, ambaye katika mchango wake kwenye makala ya Bwaya, anauliza:

Hivi kumbe kulikuwa na Jumuiya? Ndio kwanza nasikia hizi habari. Haya wale
walioaminiwa na kupewa dhamana ya kuongoza mashua hiyo wajitokeze wenyewe
hadharani tuwaweke kiti moto na kama wamechemsha basi wajitoe wenyewe wasisubiri kustaafishwa kwa manuafaa ya jumuiya.

Hoja au swali la Koero, halitofautiani sana na hoja alizotoa KISSIMA wa NDUREMO, ambaye naye nitapenda nimjibu changamoto zake alizozitoa akianzia kwa kushangaa kuwa:

Da! Kumbe kuna jumuia ya wanablog,? Ni hatua nzuri iliyokwisha kupigwa. Hivi
malengo hasa ya jumuia hii ni yapi? Viongozi wa jumuia hii wako wapi? Namfahamu
Kaka Kitururu basi. Kuna malengo gani ya baadae kuhusu jumuia hii? Mpaka
sasa jumuia hii imeshapata mafanikio gani?Ni vigezo gani vinazingatiwa ili mtu
kuwa mwanachama? Kuna kauli mbiu yoyote ya jumuia?

Lakini pia, katika makala hizo nitapenda kugusia juu ya hoja au changamoto zilizotolewa na mdau MLILIA HAKI, ambaye sijajua kuwa anapatikana kwa anwani ipi, ambaye katika mchango wake, alikuwa na haya ya kusema:

Nakubaliana na anon wa 10/3/09 2:37AM. Tatizo linaloimaliza jumuiya yetu ni la
kiuongozi zaidi. Mwenyekiti mbali na kutokufahamika kwa 'wananchi' lakini
inaelekea kuna mazingira yasiyoeleweka yaliyomweka madarakani. Kwa mfano
nilipokuwa nafuatilia kumbukumbu za mwenendo mzima wa uchaguzi kwenye blogu ya blogtanzania, nilibaini hitilafu kubwa. Uchaguzi ule ulifanyika kwa mizengwe ya
kimaslahi ambapo nahisi msimamizi wa uchaguzi huo alizidiwa na damu. Pamoja na
malalamiko mazito yaliyotolea baada ya 'upishi' wa matokeo hayo, bado jamaa
walibaki yakichekelea na kukejeli.Ndugu zangu kinachotokea sasahivi ni matokeo
ya kuchezewa kwa uchaguzi ule. Msilalamike.

Na mwingine ambaye nitapenda nigusie changamoto zake katika mfululizo wa makala zangu, ni MZEE WA CHANGAMOTO, kutoka maskani ya CHANGAMOTO YETU, ambaye katika mchango wake, aliandika kwa urefu kidogo akisema:

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.Nashukuru kaka Bwaya kwa changamoto hii.
Kwangu naweza sema machache. Kwanza ni kwamba tutahitaji kujua mipaka ya nani
anaweza kujiunga na jumuiya. Ninalomaanisha ni kuwa kwa kuwa nina imani kuwa
wanajumuiya tutakuwa na orodha mahala fulani, tunahitaji kujua kama kutakuwa na
"ratings" za blogs zetu. ni kwa kuwa kuna wenye habari za kiutambuzi,
kiuchanganuzi, kijamii, misaada ya kielimu, misaada ya kijamii kwa ujumla,
taswira na hata wapo ambao wao ni "strictly" ngono. Kwa hiyo kujua ni vipi
tutaweza kuwa na mipaka ya nani atakuwepo kwenye jumuiya na ambaye hatakuwepo ni kwanini asiwepo. Na hapo ndipo linapokuja suala alilosema ndugu Kamala hapo juu kuwa na vi-branch vya jumuiya ambavyo vuinaendana na yale muandikayo. Na hili lina ukweli maana sisi wa changamoto, utambuzi na mijadala hatuna utendaji sawa na wale wa taswira pekee. Naamini umeliona hili. Lakini pia hata namna tunavyoshirikiana (baina ya bloggers) utagundua kuwa ni tofauti. Na kuendelea kung'ang'ania jumuiya kubwa isiyo na watu wa mtazamo mmoja ni afadhali kutengeneza ndogo itakayokuwa mfano kwa wengine na namna ambavyo tutaweza kutumia uzoefu wa hii kuendeleza hiyo KUBWA.Nawakilisha na ntarejea kuendeleza mjadala kwa manufaa yetu sote.
Kama nilivyotanabaisha awali, wachangiaji walikuwa ni wengi sana, na kila mmoja alikuwa na mchango wake wenye umuhimu wake pia, na hao niliowanukuu hapo ni wachache kati ya wengi waliochangia. Niwatoe tu hofu kwa kusema kuwa, matarajio yangu ni kwa kila aliyechangia kupata majibu ya kile alichogusia, na ikiwa itashindikana, kwa maana kama nitakuwa sijajibu kikamilifu, basi uwanja utakuwa wazi kwake kwa kuniuliza na tukajadili zaidi maana MAJADILIANO NDIO NJIA MUAFAKA YA KUELEKEA MAENDELEO ENDELEVU.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Koero Mkundi said...

Heshima zenu wakubwa, mabibi na mabwana,

Nimerudi tena, nilikaa kimya ili kusoma maoni ya wenzangu.

nadhani maoni yangu yatatofautiana sana na ya wenzangu.

Mimi naona kuna haja ya kufanya mapinduzi kama yale yaliyofanywa kule kisiwani Madagasca.
Kwa nini,nimependekeza uamuzi huo mzito uchukuliwe?.....

Haiwezekani kwamba kulikuwa na Jumuiya na baadhi ya wanablog hawaifahamu, hii inaonesha ni kiasi gani uongozi uliokuwepo hauna watu makini na wabunifu.

Huu sio wakati wa kupiga soga ni wakati wa kutenda, kwani sisi kama wanablog tumekuwa mstari wa mbele kuikosoa jamii na serikali lakini tumeshindwa hata kujiongoza wenyewe, sasa tunakosoa nini?
Hii inanifanya nikumbuke hadithi ya Biblia ya kibanzi na Boriti, tumekuwa wepesi sana kuona vibanzi kwenye macho ya wenzetu il-hali tuna Boriti machoni kwetu.

Nadhani tunahitaji mawazo mapya.
Viongozi waliopo nawaheshimu sana, na ninawapongeza sana kwa kuindesha jumuiya mpaka hapa ilipofikia, sasa nawaomba wawapishe wengine ili waje na mawazo mapya.

Kusema ukweli kama sio kaka Bwaya kuuweka huu mjadala hapa sidhanai kama tungefahamu juu ya hii jumuiya, na huu ni uzembe.

Ndugu wajumbe naomba nisijengewe chuki juu ya mtazamao wangu huu..
naomba kuwasilisha.