side ads

Hongera Taifa Stars, mmekufa kishujaa

Hatimae, safari ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, ya kuusaka
ubingwa wa soka kwa wachezaji wanaocheza ligi zao za ndani, imeishia
mikononi mwa jirani zetu Zambia.

Ikicheza michuano yake mikubwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
karibu miongo mitatu sasa, Stars, imejikuta ikiaga michuano hiyo baada
ya kutoka sare ya bao 1-1 na wapinzani hao.

Sare hiyo ilimaanisha kuwa stars, kujikusanyia pointi 4 katika mechi
tatu ilizocheza ambapo ililala bao 1-0 dhidi ya Senegal, kuwalaza
wenyeji Ivory Coast 1-0, kabla ya sare na Zambia.

Senegal na Zambia, zilizoshinda mechi moja moja na kutoka sare mechi
mbili kila moja, zimesonga mbele toka kundi lao zikiwa na pointi 5
kila moja, na kuziacha Tanzania (pointi 4) na wenyeji walioambulia
pointi 1, wakifungasha virago.

Ni wazi kuwa kutolewa kwa Stars, kumetuuma sana Watanzania wengi (kama
si wote) lakini haidhuru tuna la kujivunia kutokana na kiwango
ilichokionyesha timu yetu.

Kwamba katika bara zima la Afrika, tulikuwa miongoni mwa mataifa NANE
tu, yaliyoweza kufika hapo, ni jambo la kujivunia. Kwamba hatukwenda
huko na kuwa washiriki tu, bali washindanaji, ni jambo la fahari kubwa
sana kwetu.

Ndio maana nasema kuwa, licha ya kutolewa kwetu katika hatua ya
makundi tu, Watanzania hatuna budi kujivunia kile walichokifanya
vijana wetu, ili tuwape nguvu ya kufika zaidi ya hapo. Nia tunayo,
sababu tunayo na uwezo pia tunao. Tukiamini na kufanyia kazi kila
kitu, ni wazi tutafika siku moja.

Hongera Taifa Stars, mmekufa kishujaa, mkililetea taifa lenu sifa.

--
Sent from my mobile device

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: