side ads

Hivi haya maswali hutokana na nini hasa?

Limekuwa ni jambo la kawaida sana ambalo limeshazoeleka, kuwa unapokutana na washkaji zako mitaani wanakuuliza kwanini hiki, mara kwanini kile nakadhalika.

Chukulia mfano ulikuwa unafanya kazi, unapoacha au kuachishwa kazi, watu watakuuliza kwanini umeacha au kuachishwa kazi? Kama ulikuwa na demu, mchumba, mke au rafiki na ukaachana naye, watakuuliza kwanini uliachana naye.

Kama ulikuwa unatembea kwa gari na siku ukaamua kuzurura mitaani kwa mguu watakuuliza mbona huna gari leo, na maswali mengine kama hayo. Ninachojiuliza ni kuwa mbona uulizaji wa maswali haya huzingatia upande mmoja zaidi?

Mbona unapokuwa kazini hakuna anayekuuliza kwanini unafanya kazi? Mbona unapokuwa na huyo demu, mchumba, rafiki au mke, hawaulizi kwanini unaye? Mbona unapokuwa unaendesha gari hawakuulizi kwanini unaendesha gari au kwanini ulinunua gari?

Hivi aina hii ya maswali hutokana na nini hasa?
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Anonymous said...

maswali hayo yanatokana na jinsi wewe ulivyojiweka katika jamii.
kwa tabia yako kama ulikuwa mtu wa kujikweza unapokuwa na gari lakuazima au gari la demu wako,au ulikuwa na demu ukajiweka juu halafu kesho na keshokutwa uko juu ya mawe lazima washkaji wahoji
kunaniiii?
mbona mzee sharubu zimemshuka?
upo hapo?

Anonymous said...

maswali hayo yanatokana na jinsi wewe ulivyojiweka katika jamii.
kwa tabia yako kama ulikuwa mtu wa kujikweza unapokuwa na gari lakuazima au gari la demu wako,au ulikuwa na demu ukajiweka juu halafu kesho na keshokutwa uko juu ya mawe lazima washkaji wahoji
kunaniiii?
mbona mzee sharubu zimemshuka?
upo hapo?