side ads

Goo Now Gunners!


Yeyote ambaye aliwahi kusema kuwa vijana hawa hawawezi kitu, bilashaka ni wakati wake wa kujitizama upya na kutafakari kile alichokisema, na kwakuwa mpenzi wa kweli wa michezo, asiyeshabiki, ni Yule ambaye anaweza kukiri kuwa kweli alichemka katika utabiri Fulani, bilashaka mtajitokeza na kusema jambo hivi sasa.

Hilo ndilo ninaloweza kuwaeleza wale wote ambao mwanzonina katikati ya msimu, walithubutu kusema kuwa Arsenal, safari hii, ligi ya mabingwa barani Ulaya wataisikia tu bombani, kama sio kuwa watashuka daraja.

Bilashaka mashabiki wa timu zote pinzani kwa klabu hii, hivi sasa, wanaiangalia kwa jicho la kipekee, maana sio tu kuwa imewadhihirishia kuwa ubashiri wao ulikuwa butu, bali pia wamewadhihirishia kuwa, ligi ile ina wenyewe, nao ni miongoni mwa wenyewe.

Na ndipo hapo ninaporejea kile ambacho nimewahi kukisema na ambacho ninakiamini kuwa Ligi kuu ya Uingereza, ina makocha wa aina mbili. Aina ya kwanza ni ile ya makocha wenye ujuzi wa kufundisha soka, na aina ya pili ni ile ya makocha wenye ujuzi wa kunyakua (sio kuchukua), ubingwa au kucheza katika nafasi za kushiriki ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

Kama unabisha, shauri yako…habari ndio hiyo

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: