side ads

GO BLOGING....Ujumbe kwa vijana wa kitanzania

Leo, ndani ya kipindi cha MLANGO WA DHARURA kinachoendeshwa na Radio
Clouds, iliendeshwa mada kuhusu blogging na bloggers kwa ujumla. Yapo
mengi sana yalijadiliwa katika kipindi hicho ambacho kiliwashirikisha
bw. Michuzi, aliyekuwa akiwakilisha bloggers, bw. Phares aliyeshiriki
kama mtaalamu wa masuala ya mtandao, na bw. Beda Msimbe aliyeshiriki
kama mwandishi mwandamizi.

Naamini kuwa kupitia Michuzi anaweza kutupatia msaada kwenye tuta, kwa
kufanya magumashi kiaina apate kipindi kile na akipandishe kule
maskani kwake ili wale ambao hawakubahatika kukisikia live, wajue
yaliyoongelewa. Malkia Sophia Kessy, pia anaweza kutusaidia hili
kwakuwa yuko mjengoni Kitega Uchumi pale.

Hata hivyo, miongoni mwa mengi yaliyosemwa, na wakati twaendelea
kusubiri msaada toka kwa Michuzi au Sophia, kuna kitu ambacho napenda
niseme nilikipenda sana.

Kauli ya Beda Msimbe, katika kuhamasisha hiki kizazi cha kisasa au cha
dot com kama kiitwavyo, kujitokeza kublog. "Go Blog", ndo neno
alilolitumia. Aisee, nimelipenda sana kwakweli.

GO BLOG, vijana wa Kitanzania. Go blog please

--
Sent from my mobile device

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: