side ads

DRC MABINGWA WA CHAN

Kama ulidhani kuwa kuimba na kuvalia suruali kifuani ndio jambo pekee
liwezekanalo kule Congo DRC, kwa mtawala Kabila, bila shaka unatakiwa
ujiulize upya juu ya unachokijua kuhusu nchi hiyo.

Hii ni baada ya timu ya soka ya taifa hilo kuandika historia ya aina
yake katika ulimwengu wa soka, baada ya kuibuka mabingwa wa kwanza wa
michuano ya soka kwa mataifa ya Afrika, inayoshirikisha wachezaji
wanaocheza ligi za nyumbani kwao.

DRC, ambao hawakuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikipewa uzito wowote
wakati fainali za michuano hiyo zilipoanza kule nchini Ivory Coast,
ilitawazwa mabingwa baada ya kuwagaragaza Ghana kwa mabao 2-0 katika
mechi ya fainali iliyochezwa leo.

Je, twaweza sema nini kuhusu ushindi huo zaidi ya kuwapongeza mabingwa
hawa? Je Tanzania tumejifunza nini katika mashindano haya?

Bravo Congo DRC.

--
Sent from my mobile device

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: