side ads

DJ Fetty na kali zake toka bongo


Wengi wetu tunamsikia, kupitia kituo cha radio cha Clouds FM, baadhi yetu tunamjua, baadhi yetu tunamfahamu, baadhi yetu ni ndugu yetu, baadhi ni rafiki yetu, baadhi ni jamaa na kadhalika na kadhalika. Sifa yake kubwa ni kujua kuongea. Jamani mwanadada huyu anajua kuongea. Wakati mwingine utadhani kameza betri, wakati mwingine utadhani katiwa ufunguo vile, wakati mwingine kama kala pilipili kichaa vile…eh!! Yaani kaaaaz kwei kwei

Huyu mwanadada alipozaliwa wazazi wake walimpa jina la Fatma, lakini alipokua kua hivi na kujiingiza kwenye fani, mwenyewe akajibatiza jina la DJ Fetty, na mashabiki wake nao wakalibariki, bila shaka ndio sababu amekuwa maarufu sana kwa jina hilo hivi sasa. Wengi tunajua kuwa anajua kuongea sana tu, lakini je, unajua kuwa pia ni hodari wa kuandika?

Kama ulikuwa hujui, basi chukua hiyo, na kama bado huamini basi hebu bofya hapa utaona uhodari wake katika kuandika. Karibu sana DJ FETTY
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

Anonymous said...

duh!! mwanadafada huyu kumbe katulia eeh!!

namkubali kwa kazi zake, na sasa namkubali pia yeye kama yeye