side ads

De Plaizir... Banana na Lady JD.... Huu ni mwanzo tu……….I have just returned from a promo tour in Dar Es Salaam. I would like to
thank all Tanzania people for their simpathy and good nature. I really enjoyed
my stay in Bongo and lookforward to visiting again.. SO FROM THE BOTTOM OF MY HEART, TAKE A BIG THANK YOU FROM ME... Special thank you to my dear manager Sophia Kessy without whom, i would have got lost in Tanzania.. Thank you Sophia for your management and help in my carreer we are a good team aiming to win many things... Big up to my friends Agape, Suka, Saraphia, Ruge Mutahaba, Bula, Saudi of Star TV, Mwanamboka of TBC, the EATV crew especially the Friday night live show crew... Thanks to all the media people from bloggs to radios and newspapers... My friend and guide Gadna Habash thank………………..

Hii ni sehemu ya makala aliyoiandika huyo jamaa mwenye picha yake hapo juu. Huyu jamaa bwana, nasikia alipozaliwa kule katika mitaa Fulani Fulani ya jiji la Kinshasa, wazazi wake walimpatia jina la JEAN BLANCHARD DE PLAIZIR, lakini mwenyewe baada ya kukua akaamua eti kujibatiza jina la King of Pleasure. Unajua ni kwanini hasa alijiita hivyo? Sababu ni moja tu……. Kazi yake anayoifanya ambayo imekuwa ikipagawisha watu kila alipotia maguu kuwaburudisha.

Baada ya kufanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania mwaka jana, kwa lengo la kujitangaza katika ukanda huu wa mashariki mwa bara la Afrika, na hatimaye kuvutiwa na kila alichokutana nachi nchini humu kama ambavyo alionyesha katika shukrani zake hapo juu, jamaa ameamua kutia tena maguu ndani ya Bongo kwa ajili ya kufaidi tena ukarimu wa Watanzania.

Ujio wake huo, unafanywa na kampuni change ya masuala ya Burudani inayokwenda kwa jina la S:K Entertainment, chini ya meneja wa msanii huyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, bi Sophia Kessy, aka, malkia wa bambataa. (Malkia, hivi kile ulichoniambia ni kweli nianze kuandaa suti? Hahahaaaaa, nadhani wasomaji hawajakiona hiki kipande)

Kwa mujibu wa mawasiliano niliyofanya na Sophia kwa njia ya mtandao, De Plaizir, haji kwa ajili ya kufanya show, lakini anakuja kwa ajili ya jambo kubwa sana zaidi ya hilo, ambalo ni kukuza sanaa ya muziki katika Tanzania, kwa kufanya kazi kadhaa na wasanii wa hapa nchini.

Ikumbukwe tu kuwa, alipokuja katika ziara yake ya awali, msanii huyu, alibahatika kukutana na kuvutiwa na wasanii kadhaa wa Tanzania, miongoni mwao wakiwa ni Banana Zoro na Judith a.k.a Lady Jaydee, Wambura. Na akafanya nao kazi zilizokwenda kwa majina ya KENDE KAKA, SWALI na GEM OVER.

Nikimnukuu meneja Sophia, maneno yake aliyonieleza, alisema hivi:-


ili kuonyesha heshima na kushukuru kwa suport waliopma wasanii wenzake
anakuja tena tarehe 22 yani jumapili ijayo kufanya video na wanamuziki hao
alioimba nao kwakuwa anawakubali na amefurahishwa na ushirikiano waliompa. Pia atatembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima na kuangalia namna anavyoweza kuwasaidia

Umeisikia hiyo?

Bilashaka utakuwa na mengi ya kujua kuhusu ziara yake ya awali ya mwaka jana, na habari kuhusu yeye na projects zake mbalimbali. Usiwe na shaka. Unaweza kufahamu zaidi kuhusu projects zake kwa kubofya hapa, ukapata taarifa zaidi kumhusu kwa kubofya hapa, na pia ukatembelea blogi yake kwa kubofya hapa. Lakini pia waweza kumtembelea meneja wake katika blogi yake kwa kubonyeza hapa, na ukiwa na maswali zaidi, si mbaya ukayaangusha kwa bi Sophia Kessy, kwa kumuandikia kupitia anwani ya sophia80tz@yahoo.com.

Wasanii wa Bongo mpo hapooooo. Huu ni mwanzo tu, tunatarajia makubwa zaidi maana njia imeshafyekwa kwenu kupasua anga.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: