side ads

UCHAFUZI WA DEMOKRASIA MBEYA VIJIJINI

Nina imani sana na Bunge letu Tukufu la nchi yangu takatifu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nina imani kubwa sana na sheria zinazounda na kuainisha mamlaka ya chombo hiki na nina imani na sheria zinazokilinda pia.

Hata hivyo, katikati ya imani yangu hiyo, ninajikuta nikiwa na mashaka sana, ama na baadhi ya wajumbe wa chombo hiki na hususan uadilifu wao, ama mchakato unaotumika kuwapata, ama vyote viwili kwa pamoja. Na hapo ndipo ninapojikuta nikiingia katika mkanganyiko mkubwa zaidi, ambao ni hadhi ya Bunge letu tukufu.

Ndipo hapa ninapoanza kujiuliza maswali kadhaa kichwani mwangu, miongoni mwayo ikiwa ni, Je, chombo hiki hadhi yake inaelekea wapi? Wanaotuwakilisha huko wana sababu za msingi wanazoweza kusimama mbele ya hadhara na kujivunia kuwepo kwao huko mjengoni?

Bonyeza hapa kupata uhondo zaidi….
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: