side ads

Iwapi Tanzania yenye neema?

"Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya.
Tanzania yenye neema, inawezekana"

Naam, hicho ni kiitikio ambacho kilijizolea umaarufu lukuki mwishoni
mwa mwaka 2005 na sehemu kubwa ya mwaka wa 2006. Ilikuwa chorus
iliyotumiwa na raisi wetu, mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, wakati
huo alipokuwa akiiwania nafasi hiyo na hata alipoipata.

Kilikuwa kiitikio ambacho kilipenya vichwani mwa Watanzania na
kuwashika vilivyo. Kila kona ya nchi, kila rika na kila jinsia, kila
Mtanzania, aliimba kiitikio hicho.

Miaka minne baadae, hivi sasa, ni Watanzania wachache sana wanaoweza
kuimba kibwagizo hicho. Naweza kuthubutu kusema ni wa kuhesabika, na
ni wale wenye mioyo ya chuma na akili zenye kufanya kazi kwa kiwango
kisicho cha kawaida.

Hata muasisi wake, mheshimiwa JK, imekuwa vigumu kukiimba. Sina hakika
ni kwasababu amekisahau, au kwakuwa anaandaa single nyingine kwa ajili
ya 2010.

Hata wateule walioko kwenye bendi yake aliyoiunda baada ya kupewa
ukinara, siwasikii kuimba kibwagizo hiki. Sikumbuki mara ya mwisho
nimekisikia lini kwakweli.

Na hili ndilo limenisukuma leo hii kujitokeza kumuuliza mheshimiwa JK,
(ingawa sina hakika kama anasoma'ga' blogu) maswali machache
yafuatayo. Na kimsingi, yeyote ambaye anaweza kunisaidia katika kupata
majibu ya maswali haya, ruksa kumsaidia mheshimiwa JK, kwakuwa
natambua pia kuwa he is a very busy person.

Yako wapi yale maisha bora kwa kila Mtanzania, tuliyokuwa tunahubiriwa
kipindi kile cha kampeni? Iko wapi Tanzania yenye neema tuliyohubiriwa
enzi hizo?

Uko wapi ukombozi wa Mtanzania toka katika maisha magumu ambayo
amekuwa anaishi toka alipojitambua kuwa Mtanzania? Ziko wapi zile
ajira (milioni ngapi vile?) tulizoahidiwa?

Uko wapi ukombozi wa mwalimu wa Kitanzania ambaye toka enzi na enzi
amekuwa nguzo ya kuzalisha wataalamu mbalimbali? Uko wapi ukombozi wa
mfanyakazi wa serikali ambaye kwa miaka sasa mshahara wake unaweza
kuwa sehemu ya vichekesho kama ukiwekwa katika filamu?

Iko wapi ahueni ya mtoto wa mlalahoi wa Kitanzania ambaye anapigania
kupata elimu ili aje kulitumikia taifa lake analolipenda na
kulitukuza?

Uko wapi mheshimiwa raisi utupatie majibu yasiyo ya kisiasa kwa
matatizo yetu ya kimsingi kabisa?

--
Sent from my mobile device

Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: