side ads

NAWAPENDA MARAFIKI ZANGU... LAKINI.....

Mawasiliano na marafiki zangu, imekuwa ni moja kati ya nguzo muhimu sana kwa kila ninalolifanya katika maisha yangu, na kwa hakika, najivunia kila rafiki niliyebarikiwa kuwa naye katika maisha yangu. Nimekuwa nawasiliana na rafiki zangu kwa njia ya simu, baruapepe, barua za kawaida, kuonana ana kwa ana na njia nyingine unazozijua wewe.

Hata hivyo, kutokana na sababu zangu binafsi, kwa maslahi yangu binafsi na kwa manufaa yangu binafsi pia, nasikitika kuwaeleza wengi wa marafiki zangu kuwa, nimeamua kubadili namba zangu za simu rasmi kuanzia siku hii ya leo. Wengi wa ambao niliwapatia taarifa hii walinishauri kuwa nisifanye hivyo, na napenda kuwashukuru sana kwakuwa inaonyesha kiasi gani wangali wanapenda kuzidi kuwasiliana nami.

Hata hivyo, napenda kuwafahamisha wale wote walionishauri kutobadili namba zangu za simu kuwa, ingawa ushauri wao ulikuwa mzuri na wenye lengo zuri, na licha ya kuwa kwa kawaida huwa napenda na kupokea ushauri toka kwa kila anayenishauri, mwishoni mwa siku mimi mwenyewe huwa ndio mwenye kutoa maamuzi. Na katika hili, nimeamua kuendelea na msimamo wangu huo na kwa taarifa hii basi, ni kwamba namba zangu zote za zamani za simu hazitokuwa hewani kuanzia sasa.

Ingawa nilichokifanya ni kubadili namba za simu, hii ikimaanisha kuwa nitaendelea kuwepo hewani, kwa bahati mbaya sana ni kuwa namba zangu mpya, zimegawiwa kwa watu wachache sana na ambao hawana ruhusa ya kuzigawa kwa mtu mwingine yeyote yule asiyekuwa nazo bila idhini yangu. Kwa maana hii basi ni kuwa, nitakuwa napatikana kwenye simu zangu kwa watu wachache sana.

Kwa wale ambao bahati mbaya sana hawakuwa miongoni mwa waliopatiwa namba zangu mpya, nitapenda tuendelee kuwasiliana kwa njia ya barua pepe kupitia anwani yangu ya msangirs@yahoo.co.uk, au kupitia blogi zangu za www.uchambuzi.blogspot.com, (kwa habari na uchambuzi wa masuala mbalimbali ya kijamii), www.mnasihi.blogspot.com (kwa habari mbalimbali kuhusu namna bora ya kuishi kwa furaha) na ile ya www.ujumbepichani.blogspot.com (kwa picha mbalimbali) au kwa njia ya barua za kawaida kabisa za kuandika kwenye karatasi, ambapo unaweza kuniandikia kupitia anwani ifuatayo:-

Ramadhani Msangi
S.L.P 693 – MBEYA
TANZANIA

Napenda kuwaomba radhi wale wote ambao nitakuwa nimewasababishia usumbufu kwa hatua hii nawapenda sana na Mungu awabariki kwa sana.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: