side ads

kwa wadau wa BAMBATAA.... Sophia anasema hivi...

Unamkumbuka bi Sophia Kessy, yule wa Bambataa ya Clouds FM, ambaye wakati fulani niliandika kumhusu (bonyeza hapa kusoma makala niliyomuandika binti huyu) na kisha wakajitokeza baadhi ya wadau na kuuliza nini maana ya hilo neno Bambataa?
Binti huyu kaibuka na kujibu swali hilo na yafuatayo ni maneno aliyoyatumia mwenyewe katika kujibu swali la Je, nini maana ya neno BAMBATAA?
Hi wadau nashukuru sana kwa mail zenu lakini pia kwa ushauri na maoni ambayo mmekuwa mkinipatia sitapenda kuchukua muda mrefu kukuchosha na maneno mengi ila nachoweza kusema ni kukupa jibu fupi sana la kile ambacho ulihitaji kukifahamu kuhusu maana ya neno Bambataa ambalo umekuwa ukilisikia hapa katika kipindi changu.
Ni neno kama shika taa hapa namaanisha, kupitia kipindi cha bambataa ni asili ya uafrika ambao tunauenzi muziki wetu hivyo basi kukuambia BAMBATAA namaanisha nakupa nuru ya burudani ya muziki wenye asili na vionjo ya kiafrika kutoka pande zote na kukupa mwanga au kukumwilika kutoka katika giza ulilopo la aina nyingine ya muziki wa duniani hii.
Ndio maana ambayo naona itakuwa rahisi kwako kunielewa kwa lengo la kukuza na kuenzi muziki wetu usipotee ambao unaonekana kama unasahaulika.
Ingawa kumekuwa na tafsiri tofauti juu ya neno hili. Hiki ndio nachoweza kukuambia kwa kifupi kama hujaelewa zaidi basi niandikie sophia80tz@yahoo.com au tembelea www.africabambataa.blogspot.com asanteni wadau
Haya, kwa wale walioomba ufafanuzi wa neno hilo naamini wameshampata malkia mwenyewe wa kipindi kinachotumia jina hilo, na kama bado una maswali, basi usisite kumtembelea katika blogi yake kama alivyoelekeza hapo, au kumwandikia katika anwani aliyoitoa hapo. Kuma swali wadau? naona hakuna......... mie nauliza basi, naomba mnijibu.
Hivi ingekuwa vipi kama kila mtu angekuwa anajitokeza na kujibu kile wanachosema watu kupitia blogi mbalimbali? Ingekuwa vipi kama viongozi nao wangekuwa wanatumia muda wao kujibu au kutoa ufafanuzi wa yale yanayoandikwa katika blogi zetu?
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: