side ads

Wapi Sofia Kessy.... nakati ya Bambataa!


Jamani eeh!! wajua si kila siku mtu unakuwa na la kuongea, na pale unapokuwa huna la kuongea, basi si mbaya pia ukakopa mameno kwa wenzio. Ni kwa mantiki hii basi naomba ninukuu maneno toka kwenye kule Bongo Celebrity, kwa ajili ya kumzungumzia huyo mwenye hiyo picha hapo.
" Anaitwa Sofia Kessy.Kipindi anachokiendesha kinaitwa Afrika Bambataa kupitia Clouds FM kuanzia jumatatu mpaka Ijumaa saa moja mpaka saa tatu usiku akishirikiana na DJ wake Mohamed Ally aka 2 Short.Afrika Bambataa ni kipindi ambacho kimejikita katika muziki wa kiafrika na mambo ya kiafrika" mwisho wa kunukuu.
Sasa utamu hauishii hapo. Utamu zaidi ni kuwa huyu mwanadada ni blogger, tena mzuri sana tu. Kama huamini hebu mtembelee katika kijiwe chake mwenyewe anakiita BAMBATAA. (hivi hili neno lina maana gani?).
Na wakati ukifanya hivyo, kuna blogger mwingine tena anaitwa January Makamba (sijui naye ni mtoto wa mzee wa 'Watanzania i love you jamani msinisulubu' au ni jina tu kufanana) Hata mimi sijui bwana. Labda mumtembelee kule anakolizungumzia TaifaLetu, mtapata wasaa mzuri wa kumuuliza.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 maoni:

Mkali wa Mistari said...

Huyu dada mdogo sana kumbe, ila ukimsikiliza mambo yake kule Clouds....kwakweli huwezi kumdhania. Bravo Sophia Kessy
-------------------------------
Msangi una vijimaneno na wewe....eti wapi Sophia Kessy...na kati ya bambataa......... ila ingekuwa tamu zaidi kama ungesema....wapi mamaa sophia kessy..... nakati ya bambataa....
-------------------
Halafu kweli msangi, nami nauliza bambataa maanake nini? Sifia atujibu bwana

Anonymous said...

Ebwanaeeeeeeeeee..... kweli tusaidiwe what is bambataa bwana. Maana hili neno huku mitaani lina tafsiri nyiiiiiiingi mpaka basi

mpitiaji said...

Ni vizuri wakina dada chipukizi kama hawa wanapokuwa wanafanya mambo makubwa sana kama anayoyafanya Sophia. Inasaidia kuwajengea wanawake wenzao hali fulani ya kujiamini sana.

dada ametulia kwakweli na blogi yake iko makini. Bgup kwa bloggers wote wa tanzania na hususan bloggers walio wanawake. Tunawahitaji kwa saaaaaaaaaaaana. Tunasubiri kuona blogi ya Dina wa ukweli ukweli.