side ads

Mbeya tunaadhibiwa kwa kumpiga rais mawe?


Huyu jamaa mwenye picha hapo anaitwa Idrissa Rashid. Ni Mukurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), na picha hiyo ni kwa hisani ya blogi ya Issa Michuzi. Sasa ni hivi:

Kwa muda wa wiki la pili sasa, Mkoa wa Mbeya, umekuwa ukitaabika kutokana na kutokuwa na umeme. Na ingawa wakati wa wikiendi iliyopita walijitahidi ukawaka kwa siku moja, ulipotea tena.

Wananchi wa Mbeya kila wakienda kuuliza tatizo hasa ni nini, katika ofisi za Tanesco, kila anayeulizwa hudai yeye sio msemaji. Na kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Jijini Mbeya kumekuwa kama mtaa wa viwanda kwa jinsi majenereta yanavyounguruma kwa mashindano.

Nilicho na uhakika nacho ni kuwa, kama mheshimiwa Idrissa Rashid, angekuwa ameanza kuumwa wiki lililopita, siku hiyo tu ambayo angeanza kuumwa, keshi yake tungeshasikia kuwa yuko ama India au Afrika Kusini kwa matibabu, ambako angekuwa amepelekwa hata kwa ndege ya kukodi. Tena basi kwa fedha za shirika analoliongoza ati. Lakini kuwaleta mafundi wa uhakika na vifaa vya uhakika kushughulikia tatizo la Umeme Mbeya, inakuwa ni shida. Tutafika kweli?

Anyway, pengine basi ingekuwa ni vyema yeye mwenyewe kama atasoma ujumbe huu, au msemaji wake au yeyote wa tanesco, akatueleza kwa kinaga ubaga kuwa kunani Mbeya? Kwanini hatuna umeme kwa wiki la pili sasa? Au ndio tunatakiwa kuamini kuwa tunaadhibiwa kwasababu tulimpopoa raisi wetu mawe wakati alipotutembelea?

Maana ndio yaliyoenea mtaani hayo. Na kwakuwa hatujasikia tamko lolote la maana toka Tanesco, tunalazimika kuamini hayo ati....... ni hayo tu. Atakayenuna na anune, atakayefurahi na afurahi..... ninachojua mimi ni kuwa ujumbe umefika na siwezi kuuawa kwa kusema ukweli
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

HALS said...

Hi there,
Nimekupata wangu........kama ulivyosema kuwa pengine mnaadhibiwa sababu ya kumpopoa rais wenu mawe,kwa mtazamo wangu sidhani kama mnaadhibiwa kwa hilo ila ninachoweza sema ni kuwa siku zote "adhabu ya kaburi,aijuaye maiti".
Hivyo basi kwasasa juu ya hilo,tatizo liko kwa mshikilia madaraka wa kitengo hicho cha kuwaweka 'mwangani' na kuwawezesha kutumia vifaa vingine vitumiavyo nishati hiyo...hata hivyo hawezi stuka saaaaana sababu hayumo ndani ya hilo kaburi,"unadhani atawezaje kujua adhabu yake?"
Cha muhimu muwashike kola na kulia na hao waliokaribu yenu kiutendaji ili waamke usingizini na kuwaamsha wakubwa wao na kuanza kuwajibika..ni hayo tu.