side ads

Yona na Mramba kizimbani; Ni filamu ya komedia au ya ukweli ukweli?


Filamu ndio kwanza inaanza kuingia kwenye utamu. Baada ya watu kushuhudia mwanzo wake, ambapo wale walioitwa dagaa waliweza kupandishwa kizimbani, sasa filamu hii ya EPA, inaingia kwenye utamu wake, kwa baadhi ya wanaoonekana kuwa PAPA, kuanza kupandishwa kizimbani.


Lakini kama ilivyo kawaida, Watanzania huwa hawakosi la kusema. Hivi sasa wanajiuliza, je, staring katika picha hii ataibuka shujaa au itakuwa kama zile filamu za kihindi ambazo ataring anakufa kabla picha haijaisha? Wengine wanajiuliza je, filamu hii ni ya ukweli ukweli au ni moja tu kati ya filamu kadhaa za komedia ambazo zimekuwa zikichezwa na staring wetu, kwa lengo la kuwafanya Watanzania kucheka ili kuongeza siku zao za kuishi?

Najua umenipata namaanisha nini hasa. Tuendelee kuwemo tukisubiri mwisho wake. Bilashaka ni suala la muda tu.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Bosco said...

filamu hii ni ya ukweli ukweli mr Msangi. Naamini staring JK, ataibuka shujaa wakati huu ila bado hiki haikitakuwa kigezo cha sisi kumrejesha madarakani 2010. Ale tu vya kutosha maana msimu wake ni mmoja tu.

Anonymous said...

acheni kuingilia kazi ya mahakama nyie. Watu hawa wako mahakamani sasa, tusubiri tuone sheria ikichukua mkondo wake