side ads

mpiganaji RICHARD NYAULAWA, hatunaye tena


Wadau na wasomaji wapendwa wa Jukwaa huru la Uchambuzi, asubuhi ya leo nimepokea taarifa za kusikitisha sana kuhusiana na kifo cha mheshimiwa Richard Said Nyaulawa, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini kwa tiketi ya CCM, na ambaye wakati fulani alikuwa bosi wangu katika kampuni ya Business Times Limited.
Taarifa hizi za kusikitisha sana, nilizipata toka kwa wana mtandao ambao baada ya mawasiliano ya hapa na pale, walinijulisha kuwa, mheshimiwa Nyaulawa, ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi yaliyomlazimu kwenda nchini India, kwa matibabu wakati fulani, ambapo alitembelewa na makamu wa Raisi akiwa ziarani nchini humo, alifariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Wakati tukisubiri taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu ambao ni pigo kwa kila mpenda maendeleo nchini Tanzania, kutokana na kuwa alikuwa mtu mwenye juhudi ya kuhamasisha Watanzania kujipigania maendeleo yao, kwa pamoja tumuombe Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. BURIANI MHESHIMIWA NYAULAWA. Sisi tulikupenda, lakini Muumba kakupenda zaidi yetu.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: