side ads

Buriani Mama Afrika

SHUJAA, mpiganaji, mwanaharakati, mama wa Afrika, na mwanamke wa shoka ambaye amekuwa na majina lukuki humu barani Afrika na sehemu mbalimbali duniani, Miriam Makeba, ametutoka duniani.


Mwanamama huyu ambaye ni mmoja wa wanawake wa Kiafrika, ambao dunia haitoweza kuwasahau kamwe kutokana na mchango wao katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki mwishoni mwa wiki akiwa nchini Italia, muda mfupi akiwa ametoka katika tamasha alilokuwa amealikwa kutoa burudani.


Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya shujaa huyu ambaye naamini amekufa akiwa na furaha tele nafsini mwake. Alifanikiwa kuchangia kuleta ukombozi katika bara la Afrika, kutokana na nyimbo zake, akafanikiwa kuchangia kuondoa ubaguzi wa rangi nchini kwake Afrika Kusini, kabla ya kuona harakati zake zikizaa matunda katika taifa linaloaminika kuwa taifa lenye nguvu duniani, nikimaanisha Marekani, ambako hivi karibuni, Barak Obama, ambaye ana asili ya bara la Afrika, alichaguliwa kuwa Raisi wa kwanza mwenye asili ya weusi kuliongoza taifa hilo.


Soma zaidi kuhusu mwanamama huyu kupitia viungo vifuatavyo:

- http://en.wikipedia.org/wiki/Miriam_Makeba
- http://sw.wikipedia.org/wiki/Miriam_Makeba
- http://www.leopardmannen.no/m/makeba.miriam.asp?lang=tz

R.I.P Mama Africa
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: