side ads

Arsenal yaigaragaza Chelsea.


Unaikumbuka Reli Morogoro, ambayo enzi zile iliitwa Kiboko ya Vigogo? Unakumbuka kuwa licha ya kuwa haikuchukua ubingwa ilipokuwa na jina hilo, lakini ilikuwa msumari kwa klabu za Simba na Yanga?

Kule nchini Uingereza nako kumeibuka klabu yenye haiba ya Reli ya Morogoro. Tofauti tu ni majina maana yetu hapa nchini iliitwa Reli na ile ya kule huitwa Arsenal.

Ndio. Baada ya kuwagaragaza mashetani wekundu katika pambano lililofanyika Novemba 8, mwaka huu, (soma ripoti kuhusu pambano hilo hapa) klabu ya soka ya Arsenal, imeendelea kusherehekea mwezi wa aina yake katika mwenendo wake kwenye ligi kuu ya nchi hiyo, kwa kuwachabanga matajiri wa London, yaani Chelsea kwa bao 2-1, katika pambano lililopigwa Stanford Bridge.

Ni vigumu kuuelezea ushindi huu kwa hakika, lakini itoshe tu kusema kuwa, kwetu sisi mashabiki wa klabu hii, ni ushindi wa aina yake na uliokuwa na umuhimu mkubwa sana.

Soma ripoti kamili kuhusu ushindi huo kwa kubofya hapa. Na hapa pia. Shukrani kwa Robin van Persie, alofunga mabao yote hayo mawili katika kipindi cha tofauti ya dakika tatu tu.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: