side ads

TUNAJIFUNZA KUTENGENEZA SHANGA?

Kwa siku ya leo, sikuwa na nia ya kuandika chochote kile kwasababu ningali nautafakari na kuufanyia kazi muswada wa kifisadi wa habari ambao wanaoupigia debe wanauita Muswaha wa Sheria ya Uhuru wa Habari. Hata hivyo, magazeti ya leo yamenilazimisha niandike kidogo hapa ili kuwajulisha machache sana yaliyojiri katika magazeti ya nchini Tanzania kwa siku ya leo.

Magazeti mengi sana yamezungumzia juu ya Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever) kuwa imeingia nchini Tanzania na tayari imeshachukua maisha ya Watanzania wawili huko Arusha. Magazeti ya Majira na lile la Serikali ya Habari Leo, (kwa mfano), yote yamegusia juu ya habari hiyo, ikiwa ndio habari kuu iliyotawala kurasa za mbele za magazeti husika.

Kwa upande wa Burudani ambako ndiko kidogo kuliniacha hoi, ni habari ya kuwa eti Dar es salaam kunafanyika semina ya kutengeneza shanga.... Ndio, ni SEMINA YA KUTENGENEZA SHANGA na wala hujakosea ulivyo soma, tena semina hii inaendeshwa na Wa-Ghana, waliokuja nchini kutufundisha kuzitengeneza. Soma habari hiyo zaidi kwa kubofya hapa.

Na mwisho kabisa, nasikia eti timu ya taifa ya Tanzania, yaani ile Taifa Stars, a.k.a JK Boys, ambayo iko ziarani Brazil kwa mafunzo ya mwezi mmoja, eti ilidhaniwa ni timu ya taifa ya Watoto. Soma hapa ujue kina Mwaikimba, SMG na wengineo walivyoonekana watoto huko Brazil.

NGOJA NIKAONE SEMINA YA KUTENGENEZA SHANGA KWENYE TV
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: