side ads

"Mwana wa Komba" mwenye jicho linalowaona watoto wa Mitaani

Nadhani ndio wale wale wa kule mahali hawa maana jina tu linajieleza (nadhani Ndesanjo unaelewa namaanisha wa wapi). Huyu ni dada yetu Anna Komba a.k.a Mwana wa Komba, ambaye ameamua kujiunga katika mtandao wa Wanablogi wa Kitanzania. Ilikuwa kama utani vile nilikutana naye mtandaoni siku hiyo tukaongea mambo kadhaa akaniomba nimsaidie kufungua blogi nami nikafanya hivyo, nikadhani itamchukua muda kufikiria "Atoke Vipi" lakini kumbe mwenyewe alikuwa kajipanga anasubiri tu aone njia. Dada Anna ambaye blogi yake ameiita Jicho lake Mtaani ameanza kwa kugusia tatizo sugu la watoto wa mitaani, ingawa siamini kama kuna watoto wa mitaani kweli (nitasema siku nyingine). Mtembelee na umkaribishe kwa kubofya hapa.
Share on Google Plus

About Rama Msangi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni: