JUKWAA HURU LA UCHAMBUZI
Kutangaza katika blogi hii, piga simu namba +255 713 412176 | Au tuma baruapepe kupitia anwani ya: msangirs@yahoo.co.uk | Kwa minajili ya kudumisha mawasiliano, tafadhali jisajili katika kitabu cha wageni| Asante kwa kutembelea JUKWAA la UCHAMBUZI.... karibu tena
BUNGE LETU HALIAKISI UHALISIA WA MAISHA YETU
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 7/17/2009 10:37:00 PM| Permalink

Nimesoma, kusikiliza na kuona karibu kila kinachoendelea kutoka mjini Dodoma, ambako Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa likiendelea na vikao vyake na kwa hakika, nimejiridhisha pasi na shaka kuhusu somo la makala yangu hii. Ndio, Bunge letu haliakisi hali halisi za Watanzania.

Niliwahi kuandika huko nyuma na leo hii nitarejea nilichowahi kukiandika huko nyuma, tena kwa herufi kubwa kabisa kuwa “SINA MASHAKA WALA MATATA YOYOTE YALE KUHUSIANA NA MAMLAKA, WAJIBU, HAKI NA CHOCHOTE KILE KINACHOHUSIANA NA BUNGE LETU, KWA MUJIBU WA KATIBA”. Lakini nina mashaka na wasiwasi wa hali ya juu sana juu ya watu ambao wamepewa dhamana ya kuunda chombo hiki.

Hivi wale Wabunge ambao wamekuwa wakiendelea na vikao vyao pale Dodoma hivi sasa, ni wale ambao tuliwachagua sisi kweli? Ni wale wale ambao mwaka 2005 walikuwa marafiki zetu? Ni wale wale ambao walitupigia magoti na kutusalimia wakati ule? Ni wale wale ambao tulikuwa tukipigana nao vikumbo katika usafiri wa pamoja huku mitaani tunakotoka?

Hivi wabunge hawa ndio wale wale ambao walisema kuwa wamedhamiria kutuletea maisha bora kwa kila Mtanzania? Hivi wametuonyesha kuwa hatukufanya makosa kupanga foleni ndeeeeeefu na kuwapigia kura wakati ule? Hivi wangali wanaabudu usemi wao wa ule wa wakati ule wa kwa pamoja tunaweza?

HAPANA. Binafsi sijaona kama kuna swali ambalo linastahili jibu la NDIO miongoni mwa hayo niliyoyaorodhesha hapo. Labda kwa wateule wachache sana wengi wao wakiwa ni wategemezi wa hawa wanaojiita Wabunge wetu. Ndio, kipi hasa ambacho naweza kukijibu kwa kusema NDIO hapo ilhali hakuna hata moja ambalo nimeweza kuliona miongoni mwa yale waliyokuwa wameniahidi wakati ule?

Hali ya uchumi imezidi kuwa mbaya sana. Maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha, usanii umezidi kukua kila kukicha, uhaba wa masoko bado ni kitanzi kwa Watanzania wenye kufurukuta kujiajiri, kiburi cha viongozi kimezidi kukua kwa kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele, dharau nazo zimekuwa zikichukua uelekeo huo huo. Sasa kipi ambacho kinaweza kunifanya niwape tano?

Ukiangalia kile ambacho kimekuwa kikiendelea kule mjini Dodoma, utabaini tena kwa haraka mno kuwa ni kama mchezo wa kuigiza. Maswali mengi yamekuwa ni yale yale ya enzi na enzi na majibu yake yameendelea kuwa yale yale kuwa serikali inajipanga. Bunge limeendelea kuiomba serikali, kana kwamba hiki ni chombo ambacho survival yake inategemea kufurahi kwa wakubwa walioko serikalini.

Na hata pale ambapo pamekuwa na maswali ya maana sana, ambayo ni machache sana hata hivyo, majibu yameendelea kuwa yale yale ya kisanii. Majibu mepesi kwa maswali magumu. Pale ambapo wahusika walijitahidi sana kutaka au kuthubutu kutoa majibu ya maana, basi haikuwa kwa ajili ya waliompigia kura, haikuwa kwa ajili ya Watanzania, bali kwakuwa UCHAGUZI UNAKARIBIA HIVYO WANAHOFIA KUHUKUMIWA NA WANANCHI WAO. Ndio, si wanatamka wenyewe?

Sasa niwape tano kwa lipi hasa? Kwakuwa wanajidai kuniogopa sasa hivi kwakuwa mwakani wanaogopa nitawahukumu? Yaani wameninyonga kiasi hicho na sasa wanataka kunipaka mafuta kwa maneno ya kuonyesha wananiogopa ili niwaonee huruma? HAPANA.

Yale mamilioni ya ajira ambayo tuliahidiwa, sijui hata ni kina nani ambao walau walikumbana na upepo wake? Wakulima wangali wanapigika kama hawana thamani ndani ya nchi yao, kama hawana chochote cha kuchangia katika taifa hili. Je, kuna cha kuwasukuma waipe tano serikali hawa wanaoitwa Wabunge wao?

Safari ndio kwaaaaaanza inaanza.

 
haya mambo yapo kweli au ni usanii wa hali ya juu wa wachoraji wa katuni?
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/29/2009 10:09:00 PM| Permalink

hebu jiulize
 
ubingwa umeenda brazil, walistahili, sisi tumejifunza nini?
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/29/2009 10:01:00 PM| Permalink
michuano ya mabara imemalizika kwa Brazil kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. Bilashaka walistahili, unless tu mtu uwe hukuwa na mzuka nao, lakini kwa wapenzi wengi kama si wote wa soka, kwa Brazil, kuutwaa ubingwa huo, halikuwa jambo la ajabu wala la kushangaza.
Misri, walimfunga Italia, katika pambano lao, na Afrika Kusini, waliokuwa wenyeji, walipokutana na Brazil walijitahidi hadi kufikia dakika ya 88, ndio wakafungwa bao moja katika mechi ya nusu fainali. Ni wazi kuwa matukio haya, yalikuwa miongoni mwa matukio ambayo ni ya kihistoria na ambayo yameleta changamoto katika ulimwengu wa soka, ambao ulikuwa umeelekea kama si kuhamia kusini mwa Afrika, kwa ajili ya kuona kama nchi hiyo itaonyesha kukwama na hivyo kuashiria kile ambacho kimekuwa kikihanikizwa kuwa hawataweza kuandaa fainali za dunia mwakani.
Tuyaache hayo, maana yashakuwa historia sasa. jambo la msingi ninalopenda tujadili hapa kwa pamoja ni je, sisi watu wa bara la Afrika, kwa ujumla, tumejifunza nini kupitia mashindano hayo?
 
unazifahamu fani/taaluma zenye kuwalipa waliozisomea sana? unasoma kwa malengo?
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/14/2009 09:12:00 PM| Permalink
Wengi wetu tunajua umuhimu wa elimu. Tupo tulioenda shule, tupo tuliopita shule, tupo tulioingia madarasani, tupo tuliokwepa umande… alimuradi tu, tupo wa aina kibao. Hata hivyo, licha ya kutofautiana kote huko, wote kwa pamoja tunaamini na kujua kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini swali moja ambalo pengine wengi wetu huwa hatujiulizi ni hili; Je, tunasoma ili iweje hasa?

Wengi bilashaka watasema ili waweze kuwa na maarifa ya kujiendesha kimaisha na majibu mengine mengi ya aina hiyo. Swali jingine linakuja hapo hapo; Je, huwa tunasoma kwa malengo? Jibu la swali hili bilashaka ni tete kidogo, maana ukweli ni kwamba wengi wa sisi Watanzania, ni watu ambao tumekuwa tunaenda shuleni au chuoni kwasababu tu tumepata nafasi ama kwasababu tumekosa kitu Fulani tulichokuwa tukitaka.

Katika mkondo huu ndio tunapokutana na kundi la watu ambao katika maisha yao walitamani au kuwa na ndoto ya kuwa akina Fulani, lakini wakashindwa na kuamua kuchukua njia nyingine si kwasababu ya kupenda, bali kwasababu tu ya kukosa malengo na uelekeo wa umakini. Je, hicho unachosoma wewe, ulishakipigia mahesabu na kujua kitakulipa kwa kiasi gani? Je, ni taaluma zipi ambazo hulipa sana?

Hebu pitia makala HII HAPA, ujue ni wana taaluma wepi ambao kile walichosomea kinalipa kuliko hata unavyoweza kuwaza wewe. Na pia ujue ni fani au taaluma zipi zinalipa zaidi kuliko zingine.
 
eti kila anayekufa hufa kwa mapenzi ya mungu?
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/14/2009 08:50:00 PM| Permalink

Mh!! Huyu naye amekuja kwa kasi ya aina yake jamani. Ni mwanadada anayekwenda kwa jina la Martha Noah Msangi… hahahaaaa, watu bwana…mshaanza kujiuliza maswali meeeeeengi…shauri yenu). Anyway, binti huyu ambaye ni mwanafunzi katika chuo cha Tanzania Institute of Acountant (TIA), ni mmoja ya bloggeres wapya ambao nimebahatika kusanifu jumba lake.

Wengi walikuja, wengi wakapotea, wengi tungali twajikongoja, na wengi wanafanya uzuri sana pia..… je, huyu ataangukia katika kundi lipi? Ni wa msimu au ni wa kudumu? Mimi sijui jamani. Ninachojua ni kuwa kaanza kwa kasi kubwa sana maana kaanza kwa moja ya mijadala nyeti mno. Pengine ni vyema tu kumtembelea mwenyewe katika maskani yake kwa kubonyeza HAPA, na ujaribu kumjibu swali analojiuliza yeye, mimi na wengine wengi. JE, KILA ANAYEKUFA, HUFA KWA MAPENZI YA MUNGU?
 
TANGAZO...TANGAZO...TANGAZO...KWA WAPENZI WOTE WA MK MUSIC GALAX...
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/09/2009 09:34:00 PM| Permalink
Habari Wasikilizaji wa MK Music Galaxy. Tunapenda kuwatangazia ya kwamba, kutokana na Sababu za Kiufundi Ktk Servers zetu za Linux, MK Music Galaxy haipo hewani kwa Muda huu, Tunajitahidi kadri tunavyo weza kuirudisha hewani.Kwa Sasa website tumeiweka hapa http://81.103.196.23/ kwa muda.Samahani kwa usumbufu wowote utakao jitokeza.

MK Music Galaxy - Exploring Tanzania Music.


ikiwa unahitaji maelekezo zaidi, tafadhali usisite kututembelea katika anwani yetu ya muda kwa kubonyeza HAPA, au kutuandikia kupitia anwani ya barua pepe ya: u2us@mkmusicgalaxy.com
 
NINI KILIIKUMBA Air France Flight 447, USAFIRI WA ANGA UNGALI SALAMA?
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/02/2009 02:20:00 PM| Permalink

JE, usafiri wa anga ndio njia salama zaidi ya kiusafiri kuliko nchi kavu na majini? Hili ndio swali ambalo limeiteka dunia hivi sasa, ikiwa ni takriban siku mbili na ushee sasa toka ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, iliyokuwa na abiria na wafanyakazi wapatao 228 ndani yake, ipotelee katika anga la bahari ya Atlantiki, ikiwa katika safari ya kutoka Rio de Janeiro kuelekea Paris.

Makundi ya wataalamu sehemu mbalimbali duniani wamegawanyika katika makundi madogo madogo yenye kutofautiana kimtizamo kuhusu nini hasa kilichoikumba dege hiyo, hadi kupoteza mawasiliano na waongoza ndege toka viwanja mbalimbali. Wapo ambao wangali wakijiuliza NINI HASA KILIIKUMBA NDEGE HIYO?

Wakati mtandao wa LIVE SCIENCE, ukichapisha habari ndefu kuelezea kuwa licha ya kilichotokea kwa ndege hiyo, USAFIRI WA ANGA BADO NDIO SALAMA ZAIDI, kundi jingine la wataalamu limekuwa likijadili zaidi kuhusiana na dhana hiyo ya usalama wa usafiri wa anga, ambapo wanajiuliza JE, BADO USAFIRI WA ANGA NI SALAMA ZAIDI YA NCHI KAVU? Aidha, kufuatia tukio hilo, wataalamu pia wamekaa chini na kuchanganua UWEZEKANO WA KUPOTEZA MAISHA, kwa wasafiri wa njia ya anga.


Je, ni yupi aliye sahihi zaidi ya mwenzie? Bila shaka huu ni mjadala mzuri sana wa kufuatilia kwa kina. Na wakati tukiendelea kufuatilia mjadala huu, pengine ni vyema tukajipatia ufahamu wa namna makundi ya ndege (wanyama), yanavyoweza kuangusha ndege (chombo cha usafiri ). Bongeza HAPA, kusoma taarifa hiyo. Na wakati huo huo bonyeza HAPA, kujua namna ambavyo radi, ngurumo na hali nyingine mbaya za hewa zinavyoweza kusababisha hatari kwa usafiri wa angani.

Na kwa kadiri masaa yanavyozidi kusonga mbele, tayari wataalamu wameshaanza kuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kuokolewa kwa mtu yeyote akiwa hai kutoka katika ndege hiyo. Na ikiwa hakuna atakayeweza kuokolewa akiwa hai kama wasiwasi unavyozidi kutanda, basi tukio hili litakuwa ni tukio baya zaidi kuwahi kuikumba tasnia ya usafiri wa anga tangu mwaka 2001. Soma habari kuu kuhusu kupotea kwa ndege hiyo, kupitia HAPA na habari ya kwanza kutoka jukwaani kuhusu tukio hilo, kwa kubonyeza HAPA. Kujua aina, mashirika na safari za ndege zilizo salama zaidi bonyeza HAPA.
 
228 WAHOFIWA KUFA BAADA YA NDEGE KUPOTEA
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 6/01/2009 07:05:00 PM| Permalink

Kuna wakati hapa kati kati, usafiri wa anga, ulikuwa ukichukuliwa kama ndio usafiri ambao usalama wake ni wa uhakika zaidi kulinganisha na usafiri wa nchi kavu au ule wa majini. Hii ilitokana na ukweli kuzidi iri wan chi kavu huku pia dunia ikiwa iko katika zama mpya na za aina yake za uharamia katika vyombo vya usafiri vya majini.

Lakini, tayari wadau na wadadisi wa masuala ya usafiri wameshaanza kuanza kukokotoa usalama uliokuwa ukisemekana kuwepo katika vyombo vya usafiri vya angani, kufuatia ajali za ndege nazo kuzidi kushika kasi ya ajabu. Na miongoni mwa matukio ambayo yamesukuma mchakato wa wadau na wadadisi hao, ni ajali iliyotokea leo iliyohusisha ndege aina ya Air Bus A330, mali ya shirika la ndege la Ufaransa.

Ndege hiyo inayotajwa kuwa ilikuwa na umri wa miaka mine tu, ilikuwa na abiria 216 na wafanyakazi 12, ilikuwa ikitokea Reo de Janeiro, kuelekea Paris, ambapo inasemekana kuwa ilipata matatizo wakati ilipokuwa ikikatiza katika ukanda uliokuwa na radi na ngurumo kali katika bahari ya Atlantiki. Soma habari hii kwa kina kwa kubonyeza hapa. Tizama picha ya video kwa kubonyeza hapa
 
Hatuna haja na vichwa kama hatuwezi kufikiri
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 5/28/2009 01:33:00 PM| Permalink
Dakika chache sana kabla sijaandika makala hii, nilikuwa nachat na dadangu Yasinta Ngonyani, bloga mwenye kuendesha blogi ya MAISHA. Katika mazungumzo yetu hayo mara tukaangukia katika mada ya mashindano ya urembo ambayo katika miezi kama hii, ndio wazimu wake unakuwa umeiteka Tanzania.

Tukajadili mengi japo kwa ufupi ufupi sana, na akanielekeza katika blogi ya MATONDO, ambako huko nilikutana na makala hii, kuhusu mashindano ya urembo. Maongezi baina yangu na dada YASINTA, pamoja na makala ya MATONDO, vikanirejesha katika jambo moja ambalo limekuwa likiniumiza kichwa kwa muda mrefu. Kiwango cha matumizi ya akili, fikra na kujithamini kwetu.

Nimekuwa nikijiuliza mambo hayo kutokana na mambo ambayo nimekuwa nikiyashuhudia kupitia mashindano haya ya urembo pamoja na wale dada zetu wacheza show wa bendi mbalimbali hapa nchini.

Imeshajengeka hivi sasa kwamba, katika mashindano ya urembo ni lazima dada zetu wavae nguo ambazo zamani zilikuwa zikiitwa za siri, kabla ya kuanza kuitwa za ndani hivi karibuni. Limekuwa jambo la kawaida sana hivi sasa kuwaona wale dada zetu wacheza show wakicheza wakiwa na vivazi vya aina hiyo hiyo. Kifupi ni kuwa, limekuwa jambo la kawaida kwa wacheza show na mamiss, kuvaa au sijui kuvalishwa mavazi yenye kuacha miili yao uchi kwa zaidi ya asilimia 70.

Kinachoniumiza kichwa hapa ni kwamba, hivi ni kwanini wacheza show wakaamua kufanya au kukubali kulazimishwa kuvaa mavazi yale? Hivi, kama wacheza show wa bendi zote wakiweka msimamo na kuwa wanavaa mavazi ya kiheshima zaidi, wapenzi wataacha kwenda kutizama na kuburudika na muziki wao? Na kama kina dada hao wacheza show wenyewe au wanawake kwa ujumla wao hawataki kulishikia hili kidedea na kuona wanajidhalilisha, nani awasaidie?

Vivyo hivyo kwa wanaoshiriki mashindano ya urembo? Ni lazima wavae mavazi ya vichupi? Ni lazima wajiache wazi ndio waweze kuonyesha urembo wao? Je, wakigomea udhalilishwaji wa namna ile, wizara yenye kushughulikia masuala ya kina mama ikaweka sheria kali za kukataza mavazi yale, ni nani atawatikisa? Kwanini tutumie kigezo cha kuwadhalilisha kina dada kwa ajili ya kuwapatia kipato?

Mjadala huu ni mrefu kidogo, ila kwa leo, hebu tuanze kutafakari kwa kupitia hapa. Mzee wa CHANGAMOTO, naye aliwahi kuligusia hili kwa kuandika HIVI:
 
Bravo FC Barcelona.....poleni sana Man U.
Imeandaliwa na: Ramadhani Msangi |Tarehe: 5/28/2009 12:12:00 AM| Permalink

Ilikuwa ni lazima Manchester United wafungwe katika fainali hii, na kama unataka kujua kuwa ni kwanini ilikuwa ni lazima iwe hivyo, jibu ni rahisi sana, nalo ni kwamba, yaliyojiri katika fainali hii, ni miongoni mwa mambo yale ambayo Arsene Wenger, huyaita “yenye kuufanya mchezo wa soka kuwa wa kuvutia, kuliko mchezo wowote mwingine”

Poleni sana ndugu, marafiki na jamaa zangu mlio mashabili na wapenzi wa Manchester United. Hongereni sana wale mlio mashabiki wa Barcelona, kwa kuutwaa ubingwa huo. Ilikuwa fainali ya aina yake. Fainali iliyokutanisha wachezaji wanaotawala dunia kwa sasa, Lionel Messi vs Christiano Ronaldo. Nahitajika kusema nani aliye bora jamani?? Kama hujui, basi rejea mchezo huo utapata jibu.

Pengine Patrice Evra,anaweza kutueleza sasa, kuwa je hilo lilikuwa pambano baina ya wanaume na akina nani? Maana Man U vs Arsenal, ilikuwa wanaume dhidhi ya wavulana. Ila yote kwa yote ni kuwa, Ilikuwa fainali bora kabisa ambayo mwisho wa siku ilishuhudia timu iliyo bora kabisa ikitwaa ubingwa huo.


Soma zaidi kwa kubonyeza HAPA